School Logo

Kuhusu Chuo

Simiyu Institute of Technology (SIT) ni taasisi ya mafunzo ya ufundi stadi na teknolojia iliyopo Somanda, Bariadi – Mkoa wa Simiyu, Tanzania. Taasisi imeanzishwa kwa lengo la kutoa elimu bora ya vitendo na nadharia ili kuwawezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa kwa ufanisi katika sekta mbalimbali. Tunatoa mafunzo yanayozingatia mahitaji halisi ya soko la ajira kwa kuunganisha taaluma na ujuzi wa moja kwa moja (practical skills). Lengo letu ni kumjenga mwanafunzi kuwa mbunifu, mzalishaji na mwenye uwezo wa kujitegemea. Tunatoa Kozi Zifuatazo: 📌 Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) 📌 Ufundi wa Kompyuta na Matengenezo 📌 Graphics Design & Video Production 📌 CCTV & Alarm Systems 📌 Secretarial & Office Administration 📌 English Course 📌 Ushonaji, Ususi na Mapambo Kozi zetu zinapatikana kwa muda wa miezi 3, miezi 6 na mwaka 1, kulingana na fani husika. Dira Yetu Kuwa kituo kinachoongoza kwa kutoa elimu ya ufundi na teknolojia yenye ubora wa hali ya juu katika Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla. Dhima Yetu Kutoa mafunzo bora, yanayolenga vitendo na ubunifu, ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujitegemea na kushindana katika soko la ajira.

📢 TAREHE YA CHUO KUFUNGULIWA

13 September 2026

Wanafunzi wote wanatakiwa kufika chuoni kwa wakati.